MAUJANJA KWENYE SIMU ZA ANDROID


Simu zinazo tumia mfumo wa Android zina ujanja mwingi sana. Ujanja kwenye simu za android huongezeka endapo utakuwa ume root simu yako. 

Kabla hatuja endelea ni vema nikakutajia masharti na vigezo vinavyo itajika ili kuweza kufanya maujanja kwenye simu yako ya andorid. 

Vigezo na Masharti

  • 1: Hakikisha simu yako ume root
  • 2: Mimi sita husika endapo utaaribu simu yako
  • 3: Hakikisha umeweka ES Explorer kwenye simu yako. Kama bado unaweza kui download kutoka kwenye play store kwa kutumia link chini


Leo tutaona ujanja ambao utaweza kuufanya pale utakapo edit build.prop kwenye simu yako ya andorid. Build.prop ni file ambalo lina maelezo yote kuhusu simu yako ya andorid. Maelezo kama toleo la android unalo tumia, Model ya simu unayotumia, kampuni ya simu unayotumia, mtandao wa simu unaoutumia na mambo mengine mengi. 

Fungua Es Explorer kisha slide kwenda kulia ili kupata side menu kama picha chini 

Shuka chini kabisa mpaka utakapoona kipengele kinachoitwa root explorer. Hakikisha una kiwasha hicho kipengele kama picha inavyo onekana chini 

Endapo utapata ujembe unaofanana kama picha chini basi hakikisha unabonyeza kipengele kinacho sema allow 

Ukitaka kujua file la build.prop inapatikana wapi kwenye simu yako basi fungua Es Explorer na utapata muonekano kama picha chini. 



Juu kabisa utaona kimshale cheupe pembeni ya Homepage. Kibonyeze kisha chagua kipengele kinacho sema device. Ndani ya device utaona ma folders mengi, tafuta folder linaloitwa system. Ndani ya system folder chini kabisa utaona file linaloitwa build.prop kama picha inavyo onekana chini 

Bonyeza file la build.prop kisha chagua Es Note editor kisha utapata muonekano kama picha chini 

Ndani ya file la build.prop juu kabisa utaona kialama cha kalamu kibonyeze kisha tafuta msatari unao someka 
ro.build.version.release= 
Sasa kama unataka simu yako ionekane inatumia android ya juu mfano android 6.0 basi mbele ya alama ya sawa sawa futa namba zilizopo kisha andika toleo lolote la android unalotaka liwe linaonekana kwenye about phone. Kwa mfano mimi nimeandika hivi 
ro.build.version.release=9.3 
Baada ya kumaliza juu kabisa bonyeza mshale unao onyesha kurudi nyuma ambao upo kushoto. Utapata ujumbe unaokwambia kama unataka ku save au ku discard. Bonyeza ku save kisha zina simu yako halafu iwashe. Nenda kwenye about phone utaona toleo lako la android limebadilika. Mfano mimi limeonekana kama picha chini baada ya kuweka 9.3 

Ujanja mwingine tafuta mstari unao someka 
ro.product.model= 
Mbele ya alama ya = Weka model unayotaka kama unataka simu yako ionekane model tofauti kisha save halafu zima na kuwasha utaona model ya simu yako imebadilika. 

Ujanja mwingine tafuta mstari unao someka 
ro.product.brand=
Mfano unataka simu yako ionekane brand tofauti kama Iphone au Samsung basi andika neno unalotaka mbele ya alama ya = kisha save halafu zima na kuwasha simu yako. Tazama picha chini kuona jinsi about phone yangu inavyo onekana. 

Mpaka hapo tumefikia mwisho.

Comments

Popular posts from this blog

JINSI YA KUPATA INTERNET YA BURE(HADI 1GB KWA SIKU )

NJIA RASIHI YA KUWEZA KU HACH INSTAGRAM ACCOUNT PASSWORD

JINSI YA KUHACK SMS